Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Thomas Ulimwengu leo Jumanne ya December 25 2018 amefanikiwa kusaini mkataba wamiaka miwili wa kuichezea club ya Js Saoura ya Algeria, timu hiyo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili katika timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu Algeria na iliukosa Ubingwa kwa kuzidiwa point 3 na Costantine waliyomaliza wakiwa na point 57.
Thomas Ulimwengu baada ya kusaini mkataba wa kuichezea club hiyo, sasa anaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kucheza dhidi ya Simba SC ikitokea timu yake ya Js Saoura iliyofuzu kucheza hatua ya Makundi kama Simba SC kupangwa Kundi Moja na Simba siku ya droo ya kupanga Makundi December 28 2018.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Thomas Ulimwengu kabla ya kujiunga na Js Saoura ya Algeria amewahi kucheza soka katika vilabu vya TP Mazembe vya Congo DRC, AFC Eskilstuna ya Sweden na baadae akajiunga na Al Hilaly ya Sudan aliyoamua kuvunja nayo mkataba hivi karibuni,
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati