Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba leo March 15, 2018 ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma Mjini, ambapo ndipo patajengwa Ofisi za Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji.
Tayari Rais Magufuli amekwisha toa Shilingi Bilioni 10 alizoziahidi kwa ajili ya ujenzi huo na inaelezwa kuwa ujenzi wa ofisi hizo utaanza hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa ziara yake hiyo Dr. Mwigulu ameeleza kuwa hadi sasa tayari eneo la mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo za Uhamiaji na kuongeza kuwa ofisi hizo ziko karibu na ofisi nyingine za serikali kama ya Vitambulisho vya Taifa, Zimamoto na nyingine.
Waziri Mwigulu ameeleza kuwa ofisi hizo kujengwa karibu na ofisi nyingine za serikali itasaidia wanaokwenda kupatiwa huduma kwenye Ofisi hizo za uhamiaji kuweka kupata huduma nyingine za kiserikali zilizopo karibu.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dr. Anna Makakala amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa fedha za kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote.
Ndoto anayotamani kuifanya DC wa Muheza, Ameanza na Kampeni hii