Baada ya kuwepo kwa video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadaiwa kuonesha namna mchele wa plastic unavyotengenezwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imetoa ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo.
Ayo TV na millardayo.com zinaye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Hiiti Sillo ambaye anafafanua zaidi…
>>>”Taarifa ambayo inahusu mchele wa plastic ambayo inasambazwa kupitia WhatsApp kwamba kuna mchele ambao unatokana na plastic na ambao upo katika soko na wananchi wanapikia chakula cha namna hiyo ambacho ni hatari kwa afya yao.
“Taarifa za awali tulizipata mapema mwezi huu kupitia mitandao hiyo hiyo na vile vile tukatoa taarifa kama tarehe 8 mwezi Juni tukafafanua kwamba hadi sasa hakuna mchele hasa ile brand iliyokuwa imezungumzwa wakati ule ya Basmati ambayo inaitwa Sunrice ambayo TFDA inatambua kwamba ipo katika soko Tanzania.
“Tuna mchele wa Basmati ambao umesajiliwa na TFDA na ambao upo katika soko na unauzwa kupitia maeneo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria.” – Hiiti Sillo
Aliyozungumza Bashe ndani ya dakika 10 kuhusu Bajeti Kuu 2017/18