Ivory Coast waliibuka washindi wa AFCON 2015, wakapokelewa kwa shangwe la nguvu nyumbani kwao unaambiwa mpaka Rais wao alikuwepo kuwapokea mabingwa hawa, halafu kila mchezaji akapatiwa zawadi ya pesa na nyumba za kifahari.
Moja ya story iliyochukua headlines siku ya jana kwenye ulimwengu wa michezo ni ishu ya washindi wa pili kwenye michuano hiyo, kikosi cha Ghana kwamba kila mchezaji wa kikosi hicho cha timu ya taifa amepatiwa zawadi ya nyumba pamoja na gari ya kifahari aina ya Jeep.
Bado kuna utata mkubwa juu ya taarifa hii, baadhi ya mitandao imeandika leo kwamba uongozi wa Shirikisho la Soka Ghana (GFA) wamesema kuwa bado hawajapata taarifa ya uthibitisho kutoka Serikalini kuhusu kutolewa zawadi kwa wachezaji hao.
“This is not true. Absolutely not true. As I speak with you we have not received any notice from government or the sports ministry about this“– alinukuliwa msemaji wa Shirikisho la Soka Ghana, Ibrahim Sannie.
Ghana walifika fainali na kuibuka washindi kwenye nafasi ya pili baada ya kufungwa na Ivory Coast kwa penati 9-8.
Story iliyokuwa kubwa jana ilikuwa wachezaji hao kupewa gari zenye thamani ya dola 76,000/- (sawa na mil. 140 Tshs) pia kila mchezaji kupewa dola 25,000 (zaidi ya Tshs mil. 40/-).
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook