Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo imekubali kugharamia safari ya Mashabiki wa Yanga kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ta Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns.
Wizara imegharamia Mashabiki 48 ambao watakwenda Afrika Kusini kuisapoti timu siku ya Ijumaa ya April 4 2024 kwa usafiri wa basi, hili limefanyika baada ya Yanga kuiomba sapoti Wizara.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma akiwa ameambatana na Rais wa Yanga Hersi Said.
“Asubuhi hii nimeshiriki kuwaaga wapenzi 48 wa klabu ya Yanga SC ambao wanaanza safari yao leo kwa basi kuelekea Pretoria Afrika ya Kusini kushuhudia mchezo wa marudiano wa timu yetu hii dhidi ya Sundowns utakaochezwa ljumaa ya tarehe 05/04”>>> Hamisi Mwinjuma
“Safari hii itakayowawezesha wapenzi hawa kindakindaki wa Yanga kuishangilia timu yao mubashara wakiwa uwanjani imegharimiwa kwa 100% na Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais @samia_suluhu_hassan
ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kwa vitendo na kutoa
ushirikiano kwa uwekezaji binafsi kwenye sekta ya
michezo” >>> Hamisi Mwinjuma