Ikiwa zimepita siku nne tangu itokee ajali na kuua watu kumi na mmoja 11 mkoani Kagera, jioni ya January 17, 2018 imetokea ajali nyingine katika eneo la Nyakanazi wilayani Biharamulo, ambapo Bus la SARATOGA likitokea Mwanza kuelekea Kigoma limepinduka na kujeruhi watu takribani 27.
Ayo TV na millardayo.com imempata Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Biharamulo Dr.Gresmus Sebuyoya, ambaye amethibitisha kupokea baadhi ya majeruhi waliokuwa katika gari hilo na kusema kuwa katika kituo chake amepokea majeruhi 7 na wengine 20 wamepelekwa katika kituo cha Afya Nyakanazi.
Ameeleza kuwa afya zao zinaendelea vizuri lakini hata hivyo mama mmoja hali yake sio nzuri sana hivyo wamemuwekea Oxygen na mpaka sasa hivi hakuna taarifa zozote za kifo kilichotokea.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi amesema kuwa wamezipata taarifa za ajali hiyo na kuna watu wameenda eneo la tukio lakini bado hawajampa taarifa kamili.
WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI WALIOPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KATIKA MELI.