Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba leo January 2, 2018 Mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na wanaye Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza wamekwenda kukutana na Rais John Magufuli Ikulu Dar es Salaam kumshukuru kwa kuwaachia huru kutoka jela.
Babu Seya na Papi Kocha walipokea msamaha wa Rais Magufuli kwenye Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru December 9, 2017 na kuachiwa huru kutoka gereza la Ukonga ambako walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha tangu June 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto.
Kwa upande wa Rais Magufuli, ameeleza kuwa amefurahi familia hiyo imeenda kumshukuru lakini akasema shukrani zote zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye ndiye husamehe.
Kitu Papii Kocha kamfanyia Rais JPM
Video iliyonasa Babu Seya na Papi Kocha wakitoka Gerezani Ukonga