Kutoka nchini Kenya, taarifa zinazosambaa ni kuhusu zaidi ya Madaktari 500 wa Hospitali ya Kenyatta wamefanya mgomo na kususa kufanya kazi wakishinikiza kurudishwa kazini mwenzao ambaye alimfanyia upasuaji kwa makosa mgonjwa asiyestahili.
Wiki iliyopita Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare alieleza kuwa timu ya Madaktari ilifanya upasuaji wa kichwa kwa mgonjwa ambaye hakutakiwa kufanyiwa upasuaji huo na kwamba uchunguzi ulikuwa ukiendelea ili wanaohusika wachukuliwe hatua.
Tofauti na suala hilo, Madaktari hao wanadai marupurupu ambayo wanasema hawajalipwa huku Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari nchini humo, Samuel Oroko, akieleza kuwa kumsimamisha kazi Daktari huyo ilikuwa ni uamuzi ambao hauwezi kutatatua shida zinazoikumba hospitali hiyo.
Madaktari kupitia muungano huo wanashinikiza mfumo mzima wa hospitali kuchunguzwa, ikiwemo kuboresha mfumo wa kunakili data za wagonjwa na pia kuongezwa kwa idadi ya maeneo ya upasuaji.
Taarifa Rasmi ya CHADEMA kuhusu kulazwa kwa Mbowe
Magari 10 yanayoongoza kwa kununuliwa na Watanzania