Tangu jana February 28, 2018 kumekuwa na taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na hatimaye kuthibitishwa na viongozi wa nchi hiyo kuwa serikali nchini Rwanda imeyafungia makanisa 700 nchini humo.
Inaelezwa kuwa kufungwa kwa makanisa hayo kunatokana na madai ya kuwa makanisa hayo yameshindwa kufuata miongozo ya kuanzisha na kuendesha kanisa, moja wapo ikiwa ni namna ya kujenga lakini pia yanatengeneza kelele nyingi na kusumbua wanaoishi karibu nayo.
Kiongozi mmoja wa serikali ameliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa baadhi ya makanisa hayo 700 yaliyofungwa ni ya Kipentekoste huku msikiti mmoja pia ukifungiwa.
Kwa mujibu wa sheria mpya iliyopendekezwa, viongozi wa makanisa yote lazima wawe wana elimu ya Theolojia kabla ya kuongoza makanisa. Inaelezwa kuwa wachungaji wamekuwa wakiongoza makanisa kwasababu tu wanafanya miujiza hata kama hawana elimu hiyo.
Nyimbo 13 za Bongofleva, TCRA imeagiza zisipigwe Redioni wala TV
Madiwani wawili wa CHADEMA wajiuzulu Serengeti kuhamia CCM