Leo December 22, 2017 Waziri wa Nchi ofisi ya Rais – TAMISEMI Seleman Jafo ametangaza ajira mpya kwa walimu ili kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi na walimu katika shule za Msingi na Sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi.
Akiongea na waandishi wa habari Jafo amesema baada ya uhakiki wa maombi yalitumwa, jumla 3,033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi, kati yao walimu 266 ni wa sekondari na 2,767 ni wa shule za Msingi.
Walimu watatakiwa kuripoti katika ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa na kisha kwenda kuripoti katika shule walizopangiwa, walimu wanatakiwa kuripoti December 27, 2017 hadi January 17, 2018 wakiwa na vyeti vyao,” – Jafo