Kamishna wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani amekutana na waandishi wa habari ili kutoa taarifa ya matukio yanayotukia Dar es Salaam kwa kila kipindi cha mwezi mmoja ambapo pia amegusia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Akwilina Akwilin February 16, 2018.
Katika mkutano huo, ameeleza kuwa kifo hiki kilitokea baada ya baadhi ya watu kufanya maandamano kinyume na sheria na kujaribu kupambana na polisi na polisi kushambuliwa na kupelekea wawili kujeruhiwa.
Ameeleza kuwa tukio hilo lingeepukika kama maandamano yasingefanyika, hivyo kama vyama vya siasa na vikundi vya kijamii vitaendelea kuvunja sheria na kupambana na polisi, vitasababisha jambo baya kutokea.
CP Marijani pia ameeleza watu waache kuingilia kazi ya Jeshi la Polisi katika kufanya uchunguzi mbalimbali kuhusu matukio yanayotokea nchini.
.
“Ngoja waandamane wataniona” – JPM