Application mpya kwa ajili ya huduma za usafiri ijulikanayo kama Taxify imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam huku mamia ya madereva wakijiorodhesha ili kuanza kutoa huduma hiyo katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hiyo mpya, ambayo inakua kwa kasi barani Ulaya na Afrika Taxify imetoa punguzo la asilimia 50 kwa wateja watakaotumia huduma hiyo kuanzia tarehe 08 Desemba saa tatu asubuhi.
Gharama kwa kipindi hiki zitakuwa Sh 600, Sh300 kwa kila kilometa moja, Sh 50 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Sh 3000.
Taxify inachukua asilimia 15 pekee ya mapato kutoka kwa madereva wake, ikiwa ni gharama ndogo zaidi ukilinganisha na washindani wetu wa kibiashara wanaochokua asilimia 25. Mwigizaji wa Bongomovie Wema Sepetu amechaguliwa kuwa Balozi wa huduma hii.
Ulipitwa na hii? EXCLUSIVE: Mke wa Barnaba kaonyesha Mpenzi wake mpya