Stori nayokusogezea Leo February 27, 2018 Waendesha mashtaka wa Korea Kusini wanadhamiria kumfunga miaka 30 jela Rais wa zamani wa nchini humo Park Geun-hye katika kesi ya rushwa ambayo ilimpelekea kuvuliwa madaraka.
Taarifa hizo ambazo zimetolewa na Shirika la Habari la Yonhap limeripoti kuwa Park, 66, alifukuzwa mwezi March, 2017 na ameshafunguliwa mashtaka juu ya tuhuma za rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na hata hivyo ameyakataa madai hayo.
Waendesha mashtaka hao pia wanataka Dola Bilioni 118.5 sawa na Tshs za Kitanzania Trilioni 283 kama faini kutoka kwa Park kutokana na makosa aliyoyafanya.
Mwanasheria anayemuwakilisha Rais huyo wa zamani Park Seung-gil, kwa niaba ya Park aliomba msamaha kwa kilio mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Seoul akisema Park alijaribu sana kuongoza nchi mchana na usiku.
Kauli ya kwanza ya Mbowe toka uchaguzi wa marudio
LIVE: Fatma Karume na wanaharakati wengine wa haki za kisiasa wanazungumza na wanahabari