Leo February 19, 2018 Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni nne wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kutojisajili na kupeleka taarifa za wafanyakazi wao katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ( WCF).
Wakurugenzi hao ni Abshir Gure na Farhiya Wrsame (Kampuni ya Lasar Logistic Limited), Joseph Alexander (Kamanda Security Guards Co.Ltd).
Pia Riziki Shemdoe na Deusdedit Kibassa (Kampuni ya ENCC Consultants) na Mallakhara Semis na Shafeek Purayil (Kampuni ya Spash International Co.Ltd).
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa na Mawakili tofauti akiwemo Emmil Kilia.
Akisomewa mashtaka yake, Joseph wa Kampuni ya Kamanda Security Guards Co.Ltd anadaiwa kuwa January ,26,2018 walishindwa kujisajili na kutoa taarifa muhimu za shughuli zake kwa WCF.
Kilia amedai katika kesi hiyo namba 34 ya 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi wake kwa afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Mshtakiwa Malakhara Semis na Shafeek Purayil wa kampuni ya Spash International Co.Ltd
wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi ambapo amedaili December 25,2017 washtakiwa walishindwa kusajili.
Pia walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi wao kwa Afisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF ambapo September 6,2017 washtakiwa hao walishindwa kutoa taarifa muhimu za wafanyakazi ikiwamo majina na mishahara.
Mshtakiwa mwingine Abshir Gure na Farhiya Warsame wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Emma Msofe ambapo amedai November 3,2017 walishindwa kusajili na kupelekwa taarifa muhimu kwa Mfuko wa WCF.
Amedai kuwa October 19,2017 walishindwa kutoa taarifa muhimu zikiwamo majina na mishahara.
Hata hivyo, mshtakiwa Riziki Shemdoe na Deusdedit Kibassa wa kampuni ya ENCC wameshindwa kusomewa mashtaka yao kwa sababu hawakuwepo mahakamani kutokana na kupata udhuru.
Katika kesi hizo, upande wa mashtaka umeeleza kuwa upelelezi wa kesi hizo umekamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo kila mdhamini atasaini ahadi ya Shilingi Milioni 50.
Washtakiwa hao walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa.
“KAMA WEWE NI BODABODA, KUNA HAYA YA KUZINGATIA” WAZIRI MKUU