Moja kati ya stori zilizochukua headlines katika soka la Ulaya jana ni pamoja na goli la staa wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo alilolifunga katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya UEFA Champions League dhidi ya Juventus.
Mchezo huo ulimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli mawili yakifungwa na Ronaldo na moja la mwisho likifungwa na Marcelo ila goli la kwanza la Ronaldo alilofunga kwa tiki taka ndio limeacha headlines kwa mashabiki wa soka na wachezaji ambao kila mmoja kalitolea maoni yake.
Staa wa zamani wa Man United ambaye anaichezea LA Galaxy ya Marekani kwa sasa Zlatan Ibrahimovic ambaye amewahi kufunga goli linalotaka kufanana na goli la Ronaldo ila yeye ilikuwa ni game ya Sweden dhidi ya England amelizungumzia goli hilo “Lilikuwa goli zuri lakini angejaribu kufunga vile kutokea umbali wa mita 40”
Goli la Zlatan alilofunga vs England
Goli la Ronaldo alilofunga vs Juventus
https://youtu.be/3jmw9vLK4I4
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne