Ubalozi wa Marekani Tanzania kwa kushirikiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF unakusudia kuinua industry ya filamu Tanzania ikiwatumia wataalamu wao kutoa mafunzo ya namna ya kukuza soko la filamu.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Kaimu Balozi wa Marekani Tanzania Bi. Virginia Blaser ambaye amesema lengo la ushirikiano huo ni kutaka kuinua tasnia ya Filamu Tanzania kwa kuwatumia wataalamu wa filamu wa Marekani pamoja na kudumisha uhusiano uliopo baina ya watu wa Marekani na Tanzania.
Aidha, Bi. Blaser amesema kuwa watatoa mafunzo mbalimbali kuhusu namna ya kuandaa filamu na kuzisambaza ambapo mafunzo yatatolewa kwa mara ya kwanza kwa wanawake wanaojihusisha na filamu.
MSIBA: Dogo Mfaume wa ‘kazi ya dukani’ amefariki…