Nchini England katika soka habari kubwa leo April 20 2018 iliyochukua headlines ni kuhusiana na kocha wa club ya Arsenal Arsene Wenger kutangaza kuwa ataondoka timu hiyo mwishoni mwa msimu, Wenger ataondola katika timu hiyo mwisho wa msimu baada ya kuitumikia kwa miaka 22.
Baada ya Wenger kutangazwa kuwa ataondoka club hiyo mwisho wa msimu wengi walitaka kufahamu kuwa mrithi wake atakuwa ni nani? ni wale waliokuwa wanahusishwa awali au kuna mpya, taarifa ikufikie kuwa Arsenal wameanza kuhusishwa kuhitaji hudumu ya kocha wa zamani wa FC Barcelona Luis Enrique.
Enrique ameripotiwa kuwa tayari amefanya mazungumzo ya siri na mkurugenzi mpya wa Arsenal Raul Sanllehi kukubaliana kila kitu, Enrique mwenye umri wa miaka 47 amewahi kufundisha vilabu vya Barcelona B, Celta Vigo na FC Barcelona na amewahi kutwaa mataji ya UEFA, LaLiga mara mbili, UEFA Super Cup na FIFA Club World Cup.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao