Wanasema dunia ina mambo, na ukiistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Katika jamii za Kiafrika si rahisi kuona mtoto kwenye familia hususani akiwa mdogo kufanya jambo linaloashiria kumuwajibisha mzazi wake kwa kosa lolote ambalo ametenda.
Lakini suala hili limefanyika tofauti huko wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mtoto mwenye umri wa miaka 5 akielezea jinsi alivyoamua kwenda polisi kumshtaki baba yake mzazi.
Mtoto huyo ameeleza kuwa alikwenda kumshtaki baba yake mzazi baada ya kugundua kuwa baba huyo alikuwa anapanga kuuza shamba la familia pasipo kutoa taarifa.
Mtoto huyo amesimulia mkasa huo na kueleza kuwa alikuta baba huyo akizungumza bei na mteja na ndipo alipoamua kuwahi polisi kutoa taarifa tena kwa kuomba lifti ya gari la mtu aliyekuwa anamfahamu na alipofika aliwaeleza polisi kisa kizima.
Baada ya hayo polisi, ilibidi waende nyumbani na huyo mtoto ili kuzuia mwanaume huyo kuuza shamba. Kwa mujibu wa mtoto huyo, hana mama na hivyo anaishi yeye na baba yake pekee, hivyo ilikuwa ni lazima baba yake ampe taarifa kama anafanya maamuzi ya kuuza shamba.
Jamaa aliekatwa mapanga kisa kumshika Mbuzi wa tambilko