Mahakama ya juu ya kiutawala nchini Ufaransa imekataa kumpa uraia mwanamke mmoja wa asili ya Algeria ambaye ni Muislam kwa madai kwamba alikataa kupeana mkono na viongozi mnamo mwaka 2016.
Mwanamke huyo alieleza kuwa ‘imani yake ya dini’ haikuwa inamruhusu kupeana mkono na viongozi hao pamoja na wanasiasa katika sherehe ya uraia huko Kusini Mashariki mwa Isere.
Serikali ya nchi hiyo imeeleza kuwa tabia aliyoionesha mwanamke huyo imeonesha kuwa hawezi kushirikiana na jamii ya Wafaransa na hiyo ni moja ya sababu za kutopewa uraia.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa ameolewa na mwanaume ambaye ni raia wa Ufaransa mwaka 2010.
CAG, Katibu Mkuu walivyohojiwa na Rais Magufuli kuhusu TRILIONI 1.5