Wakazi na wafanyakazi takribani 10,000 wa eneo la Berlin nchini Ujerumani wanatakiwa kuondoka eneo hilo ili kupisha zoezi la kutegua bomu la uzito wa kilogram 500, lililoangushwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia.
Inaelezwa kuwa bomu hilo liligundulika juzi jumatano, April 18, 2018. Shughuli ya kuwaondoa watu kwenye majengo yaliyoko mita 800 ilianza asubuhi ya leo April 20, 2018.
Moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa na zoezi hilo ni pamoja na kituo kikuu cha treni cha mjini Berlin. Inaelezwa kuwa idadi ya watu walioondolewa mjini Berlin ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.
BREAKING: CHADEMA wanaongea na Waandishi wa Habari