Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo June 27 2018 limetangaza rasmi kuwa limefikia maamuzi ya kuifungia miaka miwili club ya AC Milan ya Italia kushiriki michuano yoyote inayoandaliwa wa UEFA.
UEFA wamefikia maamuzi ya kuwafungiwa AC Milan kutokana na kukiuka kipengele cha financial fair play, kwa mujibu wa UEFA ni kuwa AC Milan wamevunja vipengele vinne vya financial fair play, hivyo wamefikia maamuzi ya kuwafungia miaka miwili.
Baada ya taarifa hizo kutoka AC Milan ambao wanajiandaa kushiriki michuano ya UEFA Europa League msimu ujao kutokana na kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Italia, wamefikia maamuzi ya kutangaza kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi huo wa UEFA.
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake