Kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 August 22 2018 afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura leo ametangaza mabadiliko katika ratiba ya viwanja vitakavyotumika.
Wambura ametangaza rasmi kuondolewa kwa game za Simba na Yanga kuchezwa uwanja wa Taifa kutokana na wamiliki wa uwanja huo ambao ni serikali kuwa na matumizi nao, Boniface Wambura anaeleza sababu kamili za kuondolewa kwa game za Simba na Yanga uwanja wa Taifa.
“Marekebisho katika mzunguuko wa kwanza wa Ligi, kwanza tumepata barua kutoka wizarani kuwa uwanja wa Taifa kuwa hautaruhusiwa tumika kuanzia August 22 hadi September 1 2018 kwa mechi za Ligi, kwa hiyo hizo mechi za Ligi tunalazimika kuziondoa tutazihamishia uwanja wa Uhuru”>>>Wambura
Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”