Moja kati ya habari zilizochukua headlines leo ni pamoja na tweet ya wakala Dimitri Seluk kuhusiana na mteja wake Yaya Toure raia wa Ivory Coast, Dimitri leo amepost ujumbe wa kuashiria Yaya Toure anarudi uwanjani kuendelea kucheza Ligi Kuu England katika moja ya vilabu vya juu.
Seluk amepost ujumbe unaoeleza hivi “Toure amefaulu vipimo vya afya London, Yaya anakaribia kusaini mkataba mpya, sio wa kuichezea West Ham kwa asilimia 100 Yaya ni Bingwa” Ujumbe huo umeanza kuhusisha taarifa kuwa Yaya atajiunga na vilabu vya Arsenal au Chelsea kwani ndio vilabu vikubwa vya London.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha wa Man City Pep Guardiola alimuacha Yaya Toure katika kikosi chake lakini staa huyo alimtuhumu Guardiola kuwa amemuacha kwa ubaguzi wa rangi, Seluk ambaye ni wakala wa Toure amewahi kusikika akisema Toure mwenye umri wa miaka 35 atabaki kucheza EPL ili amdhiirishie Guardiola kuwa bado ana uwezo mkubwa na alimuacha kwa chuki zake.
Kitu Mzee Akilimali kaongea kuhusu stori za Yussuf Manji kurudi Yanga SC