Simba SC leo imevunja rekodi yake mbaya dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia katika michuano ya CAF Champions League, Simba leo December 23 2018 walikuwa nyumbani uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa marudiano wa CAF Champions League round ya kwanza.
Game ya leo Simba SC walikuwa wanaingia uwanjani wakihitaji ushindi wa kuanzia goli 1-0, hiyo ni baada ya mchezo wa kwanza walioucheza Kitwe Zambia, kufungwa kwa magoli 2-1, presha ilikuwa kubwa katika mchezo huo ukizingatia Simba hawakuwahi kuwatoa Nkana mara zote walizocheza.
Simba licha ya kutanguliwa kwa goli la mapema na kupewa mzigo wa kuhitaji magoli matatu ili wafuzu, walifanikiwa kupindua matokeo na kuwafunga Nkanda Red Devils kwa magoli 3-1 na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya CAF Champions League kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 10 toka washiriki kwa mara ya mwisho.
Magoli ya Simba yakifungwa na Jonas Mkude dakika ya 29, Meddie Kagere 45 na Clatous Chama dakika ya 88 wakati Nkana walifunga goli la mapema dakika ya 17 kupitia kwa Bwalya, kama utakuwa unakumbuka vizuri Simba SC haikuwa na historia nzuri dhidi ya Nkana, toka ipoteza mara mbili tofauti na kutolewa mwaka 1994 robo fainali na mara ya pili 2002 hatua ya mtoano kama hii.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe