Leo Jumatano ya October 10 201,BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imetangaza mabadiliko na kiteknolojia kwa kuleta ubunifu kwa kuja na kadi ya malipo ya kabla (YUAN pre-paid Visa card).
Kadi hiyo ni itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China hata kama upo Tanzania pasipokuwa na pesa ya China mkononi, kwa sasa BancABC Tanzania inazo kadi 5 za malipo ya kabla ambazo zinapatikana kwa fedha ya USD, Tanzania, Uingereza, Ulaya na Afrika Kusini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kadi hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Silas Matoi alisema kuwa China imekuwa ni kati ya nchi mashuhuri kwa maswala ya biashara duniani ambapo pia wafanyabiashara wadogo na wakubwa pamoja na wanafunzi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakitembelea kwa wingi.
Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo wafanyabiashara na wanafunzi wamekuwa wakikumbana nazo. wanapohitaji fedha ya China wakiwa popote duniani.
Huduma ya kadi hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ili kulinda fedha za mteja kama kuwekwa uwezo wa kupokea ujumbe mfupi wa taarifa zake za kibenki, huduma ya kadi ya YUAN inapatikana maasaa 24 katika ATM za Visa milioni 2.7 duniani kote, kwa Tanzania ikipatikana kwenye ATM za Visa 400 na katika maduka yanayokubali kadi ya Visa 1000.
LIVE MAGAZETI: Jinamizi la MV. NYERERE latanda, Lissu atoboa majanga ya Mbowe