Club ya Al Masry ya Misri Jumatano ya March 7 2018 ilikuwa uwanja wa Taifa Dar es salaam kukabiliana na wenyeji wao wekundu wa Msimbazi Simba, katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
Al Masry wakiwa uwanja wa Taifa walifanikiwa kutoka sare ya kufunga magoli 2-2 dhidi ya wenyeji wao Simba SC, magoli ya Al Masry yalifungwa na Ahmed dakika ya 12 na Abdalraof aliyefunga kwa penati dakika ya 25, magoli ya Simba yote yamepatikana kwa penati zilizopigwa na John Bocco dakika ya 9 na Emmanuel Okwi dakika ya 74.
Ushindi huo sasa unamlazimu Simba kwenda Misri kucheza mchezo wa marudiano kwa tahadhari kubwa ya kutoruhusu goli huku akilazimika kupata ushindi wa aina yoyote ile au sare ya kuanzia magoli 3-3 ili afanikiwe kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya CAF, baada ya game kocha wa Al Masry Hossam Hassan aliongea na waandishi wa habari na kuzungumzia mchezo huo.
“Haya ni matokeo mazuri kwetu kwa mchezo wa kwanza hapa Tanzania lakini sio matokeo mazuri kwa asilimia 100 ila ni mazuri na tunamuheshimu mpinzani wetu Simba SC, ilikuwa ni game ngumu sana kwa dakika 15 za mwisho kwa sababu uwanja ulikuwa na maji na ukizingatia ni nilikuwa nacheza na wachezaji vijana zaidi”>>> Hossam Hassan
VIDEO: Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry