Leo March 8, 2018 ni Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na mitandao na vyombo mbalimbali vya habari vinazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu wanawake pamoja na ustawi wao.
Hata hivyo utafiti uliofanywa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) unaonesha kuwa asilimia 30 ya wanawake nchini wanafanyiwa ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ya kazi.
Akielezea kuhusu utafiti huo Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA Jones Majura amesema unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi umerudi kwa kasi kwa miaka ya hivi karibuni na hivyo wanawake wawe macho kutetea haki zao.
Uchunguzi uliofanya na nchini na moja Gazeti la kila pia umeeleza kuwa katika kampuni 140 nchi nzima, ni kampuni 12 tu ndizo zinaongozwa na wanawake kama wakurugenzi.
Kwa upande mwingine, takwimu za dunia kwa mwaka 2016, idadi ya wanawake wakurugenzi wa kampuni kubwa duniani imeongezeka hadi asilimia 16.
BALAA LA MVUA YA DAR: Mnara wa simu waangukia Polisi na Makazi
Kamanda wa Polisi Iringa amezungumza Abdul Nondo kupatikana