Siku moja baada ya Naibu waziri katika ofisi ya makamu wa Rais mazingira na muungano, Luhaga Mpina kufika katika bomba kuu la kusafirishia maji taka jijini Dar es salaam ambapo alikuta bomba mojawapo la majitaka likitiririsha uchafu katika maeneo ya Ikulu na kusababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira.
Leo August 06 2016 Naibu waziri, Luhaga Mpina aliendelea kufanya ziara katika maeneo ambayo yapo chini ya DAWASCO na kujionea hali halisi ya mabomba ya majitaka na baadhi ya mitambo ya kusukuma maji taka kuelekea baharini.
Naibu Waziri alibaini mapungufu kadhaa ikiwemo mashine kuharibika ambapo zinazofanya kazi ni mbili tu na moja imeharibika kwa muda wa miezi nane bila kufanyiwa matengenezo,
Aidha jenereta la akiba limeharibika kwa miaka miwili bila kutengenezwa ambapo maji yakifika kwenye pumping station yanafurika na kwenda kwenye makazi ya watu na yanaungana na maji mengine ya mvua na kusambaa maeneo mengine mbalimbali.
Baada ya kubaini mapungufu hayo naibu Waziri Luhaga Mpina amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC kumuandikia hati ya zuio la muda wa siku saba Mkurugenzi Mkuu Dawasco kuelezea kwanini DAWASCO imeshindwa kutoa huduma stahili ya maji taka licha ya wadau wanaohusika wanachangia tozo zinazotakiwa kila mwezi.
ULIKOSA HII YA DAWASCO KUMKWEPA NAIBU WAZIRI, AWAPA SIKU 14 KUTIMIZA HAYA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI