Club ya FC Barcelona hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Ligi Kuu Hispania msimu huu wakiwa wamecheza jumla ya game 31 na wameshinda game 24 na kutoka sare game 7 pekee, kitu ambacho kinaleta dalili nzuri na muelekeo mzuri katika mbio za kutwaa taji lao la 25 la Ligi Kuu Hispania LaLiga msimu wa 2017/2018.
Ushindi huo umeifanya FC Barcelona kuongoza Ligi kwa tofauti ya point 11 dhidi ya Atletico Madrid anayewafatia nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 68 na Real Madrid akiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na jumla ya point 64.
Bila kujali matokeo ya timu nyingine FC Barcelona anahitaji point 14 ili atangaze Ubingwa wa LaLiga mapema msimu huu sawa na kupata ushindi katika game 5 wakati huu akiwa kasalia na game 7 za LaLiga mkononi, kufuatia dalili hizo inaelezwa kuwa kuna uwezekano Barcelona akacheza El Clasico dhidi ya Real Madrid akiwa tayari katangaza Ubingwa wa LaLiga.
Waandishi wa habari wa Marca wameongea na kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuuliza ikitokea FC Barcelona akatangaza Ubingwa mchezo mmoja kabla ya kukutana nao, ataruhusu wachezaji wake waiweke Barcelona ‘Guard Of Honour’?
“Sijui kwa nini unaniuliza swali kama hilo lakini kiukweli mimi msimamo wangu huko wazi kabisa siwezi kuruhusu wachezaji wangu waiwekee Barcelona ‘Guard of Honour’ kwani Barcelona ndio walivunja huo utamaduni, hata hivyo bado mbali sana hadi Ligi kumalizika”>>>Zidane
Zidane amefikia maamuzi hayo ya kutoruhusu wachezaji wake waiwekee Barcelona Guard of honour ikitokea imetwaa Ubingwa wa LaLiga kutokana na kitendo cha Barcelona kukataa kuiwekea Real Madrid ‘Guard Of Honour’ wakati walipotoka kutwaa club Bingwa dunia.
Kama hufahamu Guard of Honour sio sheria bali huwa ni kitendo cha kiuungwana (fair play) kwa wachezaji wa timu pinzani kusimama pembezoni na kumpigia makofi timu ambayo imetoka kutangaza Ubingwa mchezo mmoja kabla ya kukutana nao, hivyo wanaipigia makofi ikiwa inaingia uwanjani kabla ya kuanza mchezo.
VIDEO: Canavaro baada ya game amezungumzia ishu ya kustaafu