Siku moja baada ya wekundi wa Msimbazi Simba kupoteza point mbili katika uwaja wa Samora Iringa dhidi ya Lipuli FC ya mkoani hapo, kutokana na dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 na kuishia kugawana point moja moja.
Leo April 22 2018 wapinzani wao Yanga nao walikuwa wana game nyanda za juu Kusini katika mkoa wa Mbeya dhidi ya Club ya Mbeya City, Yanga walikaribishwa na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine kucheza mchezo wao wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018.
Mchezo umekuwa kama ulivyokuwa unatarajiwa kuwa ni mgumu kwa timu zote mbili, hadi dakika 90 zinamalizika game ilikuwa 1-1, licha ya Yanga kuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 58 kupitia kwa Raphael Daudi, umakini wa beki yao ulikuwa mdogo na kufanya Mbeya City kusawazisha goli hilo dakika za nyonge kupitia kwa Idd Suleiman.
Kwa matokeo hayo saa Simba na Yanga zote zinakuwa zimepoteza point mbili katika mikoa ya nyanda za juu baada ya sare hizo, hivyo game inayofuata ni dhidi yao April 29 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam huo ni mchezo ambao timu zote zitataka kupata matokeo chanya ili kujiweka pazuri katika kuwani Ubingwa wa VPL 2017/2018.
https://youtu.be/q9HMnLDKxXQ
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao