Kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems baada ya kikosi chake kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup 2019, sasa ametangaza rasmi kukiondoa kikosi hicho visiwani humo na kukipeleka Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Js Saouro.
Aussems ameeleza kuwa kwa sasa licha ya timu yake kupata ushindi mwembamba dhidi ya KMKM kwa goli 1-0 tena kwa tabu, amesema hajali kuhusiana na matokeo anachojali ni jeraha la mchezaji wake Erasto Nyoni aliyeumiwa goti lake la kulia, hivyo kwa sasa Simba inaondoka na italeta team B.
HOFU YATANDA: Erasto Nyoni wa Simba katolewa na machela kashindwa kutembea