Club ya Yanga leo Jumanne ya January 16 2018 imetangaza good news kwa mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania, baada ya uongozi wao kutangaza club yao kuingia mkataba wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya vifaa vya michezi ya kiitaliano ya Macron.
Yanga leo wametangaza kufanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Macron, mkataba ambao una thamani ya Tsh Bilioni 2 lakini zinaweza kupanda kulingana na mauzo ya jezi, hivyo Yanga sasa imefanikiwa kumpata mdhamini rasmi wa jezi.
Mkataba huo wa Yanga na Macron, unakuwa ni miongoni mwa mikataba ambayo Macron wameingia na baadhi ya vilabu vya Afrika lakini Macron wamedhamini vilabu mbalimbali vya soka duniani kama Crystal Palace na Stoke City zote za Ligi Kuu England.
TFF imetangaza kumfungia Obrey Chirwa wa Yanga