Chama cha soka Ulaya UEFA leo kikiwa kinachezesha droo ya kupanga makundi ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019, imetangaza pia list ya wachezaji waliofanya vizuri msimu wa 2017/2018 katika michuano ya UEFA Champions League.
UEFA limewatangaza wachezaji wanne waliofanya vizuri upande wa golikipa, beki bora wa msimu, kiungo bora wa msimu na mshambuliaji bora wa msimu wa UEFA Champions League ambapo walikuwa wanagombania Lionel Messi wa FC Barcelona na Mohamed Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo.
Washindi wa tuzo hizo ni Kyler Navas wa Real Madrid ndio ametangazwa kuwa golikipa bora wa msimu 2017/18, Sergio Ramos wa Real Madrid ndio beki bora wa msimu, Luka Modric wa Real Madrid ndio kiungo bora wa msimu na Cristiano Ronaldo ndio mshambuliaji bora ambapo msimu uliopita aliichezea Real Madrid na sasa anaichezea Juventus ya Italia.
Luka Modric wa Real Madrid ndio ametangazwa kuwa mchezaji bora wa UEFA kwa wanaume kwa msimu wa 2017/18 #UEFAAwards #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/Bazw1ttfLx
— millardayo (@millardayo_) August 30, 2018
Staa wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye msimu uliopita aliichezea Real Madrid ndio mshindi wa tuzo ya mshambuliaji bora wa UCL msimu wa 2017/18 #UEFAAwards #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/bsaOXtg8AI
— millardayo (@millardayo_) August 30, 2018
Kiungo wa Real Madrid Luka Modric ndio ametangazwa kuwa kiungo bora wa UCL msimu wa 2017/18 #UEFAAwards #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/228D1n3oP7
— millardayo (@millardayo_) August 30, 2018
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos amechaguliwa kuwa beki bora wa UCL msimu wa 2017/18 #UEFAAwards #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/iEIzvwCmad
— millardayo (@millardayo_) August 30, 2018
Golikipa wa Real Madrid Keylor Navas ndio amechaguliwa kuwa golikipa bora wa UEFA msimu wa 2017/18 #UEFAAwards #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/lzr23qO1GV
— millardayo (@millardayo_) August 30, 2018
Kitu Mzee Akilimali kaongea kuhusu stori za Yussuf Manji kurudi Yanga SC