Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa anaichezea club ya Nantes ya Ufaransa Emiliano Sala, ameripotiwa kupotea kwa ndege yao binafsi aliyokuwa anasafiria kutoka Nantes kwenda Wales kuanza kuitumikia timu ya mpya ya Cardiff City.
Emiliano Sala mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Cardiff Jumamosi hii akitokea Nantes inadaiwa amesajiliwa baada ya timu hiyo kumkosa Mbwana Samatta kutoka KRC Genk, ndege aliyokuwa amepanda Emiliano Sala ilipotea usiku wa jana ikiwa katika pwani ya Guemsey.
Ndege hiyo binafsi ilikuwa na watu wawili Emiliano Sala na rubani ambapo mamlaka ya anga na wanaohusika kuitafuta ndege hiyo iliyopotea kwenye rada ikiwa Guemsey, wanatajwa kuwa hawatarajii kuwakuta abiria watu hao wakiwa hai kutokana na kudai kuwa hata kama ndege imeangukia baharini lakini hawezi kuwa hai kutokana na hali ya hewa ya sasa kuwa baridi sana.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”