Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Leo February 19, 2018 amemsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Alphonce Sebukoto kutokana na upotevu wa Milioni 279 alizoruhusu zilipwe kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwenye Account yake Binafsi, kwa kazi ya ukandarasi.
Amechukua hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya Milioni 279.
Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Sebukoto leo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
“Mwanasheria utasimama kazi kuanzia leo na tuhuma zako zitachunguzwa kikamilifu na vyombo husika na uchunguzi ukibaini kama huna kosa utarudi kazini. Hatuta kuonea lakini hatuwezi kukuvumilia kwa utaratibu huo ulioufanya.” –Majaliwa
Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema fedha alizolipwa Bahebe zingeweza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.
“KAMA WEWE NI BODADABODA, KUNA HAYA KUZINGATIA” WAZIRI MUU