January 4, 2018 Benki Kuu ya Tanzania ‘BoT’ ilitangaza kuzifungia Benki 5 na kuziweka chini ya mufilisi kutokana na kukosa mtaji na fedha za kutosha kujiendesha.
Kama unakumbuka ilitangazwa kuwa wateja hao watalipwa fedha zao ambapo malipo yasiyozidi Milioni 1.5 hutolewa na bodi ya BIMA ya Amana, hii ni kutokana na kuwa kila benki hukata bima kwa ajili ya wateja wake na hutakiwa kulipa asilimia 0.015 ambayo hutumika kwenye malipo ya awali na baadaye wakishatathmini mali na madeni ya benki wanaziuza kupata fedha taslimu kuwalipa wanaoidai hasa walioweka fedha nyingi.
Sasa unaweza kujiuliza itachukuwa muda gani wateja kulipwa pesa hizo, Tunaye Mkurugenzi wa bodi ya Bima ya Amana, Emmanuel Boaz kwenye huu ufafanuzi
HAMISA MOBETTO KAFUNGUKA MAHAKAMA KUMSULUHISHA NA DIAMOND “UGOMVI WA FAMILIA UACHENI TU”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA