Shirikisho la soka Tanzania TFF March 15 lilitangaza adhabu ya kumfungia maisha kujihusisha na soka makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.
Baada ya adhabu hiyo kutolewa Wambura alikata rufaa na kuomba kamati ya rufaa imtendee haki ndipo leo ilipoita waandishia chini ya mwenyekiti wake Ebeneza Mshana na kutangaza kuwa wameridhia Wambura aendelee kutumikia adhabu hiyo.
Enzi Samatta alivyokuwa anapiga chenga wachezaji wanne na kufunga VPL