Baada ya staa wa timu ya taifa ya Morocco Nordin Amrabat kuonekana katika picha za video akitoa lugha ya matusi kuhusiana na teknolojia ya VAR (Video Assistant Referee) kwa kudai kuwa inazipendelea timu kubwa.
Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria John Obi Mikel ametoa nae ya moyoni kuhusiana na teknolojia hiyo, Obi ameeleza kuwa VAR anaona kama inapoteza lengo la kufanya maamuzi sahihi na badala yake anaona kama inatumika kuzipendelea timu kubwa.
Licha ya wengi kutarajia kuwa uingiaji wa teknolojia hiyo katika soka utapunguza lawama kwa waamuzi lakini inatumika kwa mara ya kwanza katika World Cup 2018 na kuonekana kuwa na lawama
“Aaagh sitaki kusema chochote kuhusiana na VAR sijui ipo kwa ajili ya mataifa makubwa au mataifa madogo sitaki kusema chochote tena sina cha kusema unaweza kupiga hesabu mwenyewe na kufahamu hicho ndio pekee ninachoweza kusema”>>>> Obi Mikel
Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake