Katika kuinua uchumi wa nchi mbalimbali, nchi takribani 44 Barani Afrika zimeweka sahihi ya kutengeneza makubaliano ya biashara huria ndani ya miezi 18 kama jitihada za kuinua maendeleo ya biashara barani humu.
Makubaliano yaliyopewa jina African Continental Free Trade Area (CFTA), yalitiwa sahihi jana March 21, 2018 katika Mkutano wa nchi za Jumuiya ya Afrika (AU) mjini Kigali Rwanda.
Inaelezwa kuwa kama makubaliano hayo yatafanyiwa utekelezaji, umoja huo ndio utakuwa mkubwa zaidi wa Biashara Huria duniani kuwahi kutokea kutokana na kuwa na wanachama wengi wanaouunda.
Hatimaye Upelelezi kesi ya Viongozi wa Simba Aveva, Kaburu umekamilika