Rais John Magufuli leo October 7, 2017 ametangaza mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri. Mabadiliko hayo ni pamoja na kuongezeka kwa wizara mbili na kufanya jumla ya wizara 21 na mawaziri 21 kutoka 19 ilivyokuwa mwanzo.
baadhi ya mabadiliko hayo ni Dr. Hamis Kigwangala kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Wizara ya Utumishi imeshikwa na George H. Mkuchika, Nishati Medard Kalemani na Naibu wake Subira Mgalo, Waziri Angellah Kairuki na Naibu wake Haruni Nyongo wakiwa Wizara ya Madini huku Suleiman Jafo akipewa Wizara ya Tamisemi.
Ulipitwa na hii? Rais Magufuli ametaja mshahara wake leo