Moja kati ya habari zilizochukua headlines leo ni ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kwa kuonesha Yanga kuwa itacheza game 11 mfululizo za mzunguuko wa kwanza wa Ligi uwanja wa Taifa.
Kitu ambacho baadhi ya watu wamekizungumzia akiwemo afisa habari wa Simba Haji Manara, kati ya game hizo 11 Yanga atakuwa nyumbani game saba na game nne atakuwa ugenini ila atacheza uwanja wa Taifa kutokana na timu anazocheza nazo zinatumia pia uwanja wa Taifa kama uwanja wa nyumbani.
Haji Manara kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake kuhusiana na ishu hiyo “Haijawahi kutokea kokote duniani toka Ulimwengu umeumbwa!! Klabu moja kucheza mechi 12 mfululizo kwenye kituo chake..usisahau JKT, Simba, KMC na Lyon zitachezewa Taifa, Hoja hapa ni nini?jambo hili lingekuwa kwetu Gongowazi wangesema TFF hii ni Simba”
“Sisihatulalamiki tunakumbushana tu, hata hili la kufungiwa Meneja wetu ingekuwa wao wangehoji why Meneja wao hajafungiwa ?wakati makosa ya kina Kichuya ndio aliyoyafanya Toto? Soma bila jazba utanielewa nimemaanisha nini!! Narudia hatulalamiki ila isije tokea kwetu halaf nisikie fyoko fyoko..Ndegelec!!!”
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe