Mwanamuziki mkongwe na maarufu Afrika Mashariki na Kati ambaye alikuwa anatokea nchini Kenya Gabriel Agoya Omolo anayejulikana kwa wimbo wake maridhawa wa ‘Lunchtime’ wimbo ulioimbwa mwaka 1970 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Busia nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo cha Gabriel Omolo zimetolewa na mke wake Alice Adeya jana January 3, 2018 akimwambia rafiki wa mume wake Charles Makawita ambaye nae alizaliwa na Gabriel Omolo katika kijiji cha Nyabeda.
“Mke wake aliniita jioni ya jana niende hospitalini, baada ya kugundua hali ya mumewe inazidi kuwa mbaya”- amesema Charles Makawita
Kulingana na gazeti la Daily Nation, Omolo ni mzaliwa wa kijiji cha Nyabeda eneo la Ugunja, Jimbo la Siaya ambako alilelewa pamoja na rafiki yake Makawita.
Omolo alikuwa na uwezo mzuri wa uimbaji kwenye bendi ya Equator Sound miaka ya 1960s alikoshirikiana na Daudi Kabaka, Fadhili William na Nshil Pichen, raia wa Zambia na Peter Tsoti.
Omolo ni mwanamuziki pekee kutoka Kenya aliyewahi kushinda tuzo ya kimataifa ya International Golden Disc mara mbili mwaka 1974 na 1976 kwa wimbo wake wa ‘Lunch time’
Alikuwa mwanachama wa bendi za Eagle Blue Shades na Komesha.
BARUA ALIYOIPOKEA LEO JPM TOKA KWA RAIS MUSEVENI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
KAULI YA CHADEMA TOKA NAIROBI KUHUSU MKE WA KENYATTA KUCHANGIA MATIBABU YA LISSU