Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amempa Mkandarasi siku saba arekebishe barabara ya Keko ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wakazi wa Temeke.
“Hii ni barabara ambayo ipo kwenye mpango wa kupita magari yaendayo kasi, moja ya makubaliano katika mkataba ni kufanya marekebisho madogomadogo na tayari TANROAD wamewakabidhi, hatuwezi kukaa kusubiri, nimewapa siku 7 Wakandarsi watengeneze ili wananchi wa TMK waendelee na kazi zao” Gondwe
“Magari yanaharibika, madereva wanafukuzwa kazi na boss wao wanasema spring zinaharaibika, wanachelewa kazini ubovu huu wa barabara ndio unawachelewesha, TANROAD wameshawaandikia barua nimewaleta waone kero wanayopata wananchi mpaka Alhamis barabara ipite” Gondwe