Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameshiriki Mkutano wa Dunia wa Maji ambao unafanyika Jijini Brasilia nchini Brazil.
Mkutano huo umejadili mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya maji duniani ikiwa ni pamoja na namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuwezesha miradi ya maji katika nchi zinazoendelea.
Prof Mkumbo alikuwa moja ya wazungumzaji katika mkutano huo na ametoa tamko kwa niaba ya serikali ya katika kuboresha upatikanaji wa maji nchini na hii ni pamoja na kuwekeza zaidi rasilimali fedha katika sekta hiyo.
Ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania imeweka suala la uwekezaji kwenye sekta ya maji kuwa ni moja ya maeneo ya vipaumbele na kuhakikisha ifikapo mwaka 2021 inakuwa imefikia mahitaji ya maji kwa ukaribu na kwa uendelevu.
BREAKING: Polisi kuhusu tukio la Afisa wa Syria kushambuliwa DSM