Mabadiliko kadhaa yamefanywa nchini Ufaransa na Rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron katika sekta ya elimu katika suala la muda wa watoto kuanza shule.
Rais Macron ametangaza watoto wenye miaka mitatu kuruhusiwa kuanza shule jambo ambalo linafanya nchi hii kuwa ndio inayoruhusu watoto wa umri mdogo zaidi kuanza shule katika bara zima la Ulaya.
Rais huyo ameeleza kuwa mabadiliko hayo yanalengo la kupunguza kutokuwepo usawa katika elimu, kutokana na kwamba wazazi ambao ni maskini hushindwa kuwaandikisha watoto wao shuleni mapema.
“Wananchi wanashangilia bila kujua lile ni bomu” – Mwenyekiti CCM Mtwara