Titanic ilikuwa meli ya Waingereza ambayo ilizama katika eneo la Kaskazini mwa bahari ya Atlantic mile 400 kutoka Kusini mwa Newfoundland Canada mnamo April 15, 1912 majira ya saa 8:20 usiku.
Inaelezwa kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba abiria takribani 2200 na takribani watu 1500 walipoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Meli hii ambayo ilikuwa na uzito wa tani 46000 ilianza safari April 10, kutoka Southampton Uingereza kuelekea New York nchini Marekani, safari ambayo ilikuwa ni ya siku kadhaa baharini na hakuna aliyedhani safari hiyo isingefika mwisho.
Meli hiyo ambayo ilikuwa inamilikiwa na Joseph Bruce Ismay ilikuwa ya kifahari sana kwa kipindi hicho, ndani yake ilikuwa na migahawa ya kifahari, maktaba, swimming pool, gym, pamoja na saluni za kunyoa mbili.
Kwa kipindi hicho cha mwaka 1912 meli hiyo ilikuwa na gharama ya Dola za Marekani milioni 7.5 ambayo kwa sasa ni zaidi ya dola milioni 400 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 960.
Baada ya kupita katika vituo kadhaa ikiwa ni pamoja na Cherbourg Ufaransa na Queenstown Ireland, April 14 majira ya 5:40 usiku meli hiyo iligonga mwamba wa barafu katika upande wake wa kulia.
Mgongano huo ulisababisha kupasuka kwa upande huo na kulipelekea maji kuanza kuingia ndani ya meli hiyo na upande huo wa kulia kuanza kuzama taratibu.
Ilichukua saa mbili tu hadi meli hiyo yote kuzama kabisa baada ya kuwa imekatika vipande viwili….
Vifaa vya kuokoa maisha havikuwa vya kutosha hivyo kutokana na sera ya kusaidia wanawake na watoto kwanza, watu wengi walizama kwenye meli hiyo bila kuokolewa.
Hii ni moja ya ajali kubwa sana kuwahi kutokea duniani ambayo iligharimu uhai wa maelfu ya watu, mali pamoja na bidhaa.
Hiyo ni historia fupi ya ajali hiyo ya meli ya Titanic ambayo ilitokea miaka 106 iliyopita na hadi leo ajali hiyo inazungumzwa.
Alichoagiza Rais Magufuli kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu