Mwanamke mmoja nchini Uganda anayefahamika kwa jina la Ann Grace Aguti, amewachukiza Wazazi, Viongozi wa Dini na Jamii yake baada ya kuwaoa wanaume watatu na kumpa kila mmoja wao nyumba moja kati ya saba anazomiliki, kwa sasa ana mimba na bado hajamtaja muhusika wa mimba hiyo.
“Baba mimi ni Mtu mzima ambaye nina maisha yangu ni haki yangu kuwa na Wanaume watatu ambao wote wanaelewana bila ugomvi, ni nani kati yenu nyie Viongozi wa Dini na hata wewe Baba atanifanya kuwa Mke, kama mtalazimisha kuwafukuza Wanaume wangu watatu niliowaoa”-Ann baada ya Baba kutishia kuwafukuza Wanaume wake.
“Natamani kuwa na Mume atakayenihudumia kama Mke, ina raha yake ila sijabatika, Mume wangu wa kwanza niliyezaa nae Watoto watatu alikuwa Marioo nikamuacha kisa alizidisha wivu, nimewaoa hawa Wanaume watatu, nawalisha nimewapa kila mmoja nyumba, ila bado natafuta Dume atakayeweza kunigharamia anaweza hata kuwa Mume wa nne ”-Ann Grace