Jumla ya Waandisi 25 kutoka Tanzania wamepelekwa nchini China kwa mafunzo ya Mwezi mmoja ikiwa ni mwendelezo wa Kampuni ya Ujenzi ya Group Six International limited kuwapeleka nchini humo waandisi katika mafunzo ili kujiongezea ujuzi katika shughuli za ujenzi wa miradi mikubwa na usalama wakiwa pahala kwa kazi.
Akizungumzia safari hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa Group Six international limited, Mr Wu Wein bin amesema kuwa mafunzo hayo yamefadhiliwa na Serikali ya China kwa waandisi hao wakitanzania ili kupata ujuzi katika uhandisi na kuewongezea ufanisi na jinsi ya teknolojia ya ujenzi ilivyokuwa.
Ameeleza kuwa mahusiano mazuri kati ya Tanzania na China yamepelekea Serikali ya China kutoa Ufadhili huo ili Watanzania hao kwenda nchini humo ili kupata ujuzi jinsi ya kusimamia miradi mikubwa ikiwemo barabara, madaraja na Majengo makubwa na kujionea teknolojia mpya “- amesema Bin
“Dhumuni la Group Six international kwa kushirikiana na Chongqing Vocational Institute of Engineering ya nchini China ni kutoa mafunzo kwa waandisi wapatao 300 wa kitanzania na mwaka huu 2023 ni hao waandisi 25 ambao watapata mafunzo ya Mwezi mmoja na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia” alisema Mr Bin.
Akiongea mmoja wa wafaidika wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) Dk, Shija Kazumba ambaye anaelekea nchini China kwa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yana tija kubwa wa watanzania.
Aidha Dk.Kazumba amesema mbali na kusoma pia tutapata fursa ya kwenda kuona jinsi gani wenzetu walivyokuwa mbele kwenye teknolojia na usimamizi wa miradi mikubwa.
Naye kwa upande wake Msanifu Majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania Anna Soya amesema kuwa fursa waliopata ni chachu kwao kwenda kuona jinsi wenzetu wenzetu wenzetu walivyoweza kujenga na kusimamia miradi mikubwa.
“Mafunzo haya yatatujengea uwezo wa kuweza kusimamia miradi mikubwa ambayo ipo na ambayo itajengwa hapa hapa nchini iliwemo madaraja, barabara na majengo makubwa”, amesema Msanifu Majengo huyo.
Mpango huo wa kuwapeleka nchini China kwa mafunzo yameanza kufanyika toka mwaka 2018 na Kampuni ya ujenzi wa Group Six international limited ndio wanaratibu mafunzo hayo.