Kampuni ya utengenezaji wa bunduki maarufu nchini Marekani Remington Outdoor, imeomba msaada wa kinga dhidi ya kufilisika kutokana na hali yake ya kifedha kwa kipindi hiki.
Kampuni hiyo ambayo ilianza kufanya kazi miaka 200 iliyopita, imeomba kinga hiyo kutokana na mauzo yake kushuka sana, jambo lililotengeneza hofu ya kufilisika.
Inaelezwa kuwa kufilisika huko kumechangiwa sana na mikakati mbalimbali na maandamano yanayoendelea ya kushinikiza sheria mpya ya kudhibiti matumizi ya bunduki nchini humo.
“Lengo sio kuminya uhuru wa maandamano kwani yapo kikatiba” – Mwigulu