Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba leo February 13, 2018 amewatembelea wafanyabiashara ndogondogo katika Soko Kuu la Wilaya ya Iramba, madereva pikipiki, daladala na makondakta walio katika Stendi Kuu ya Mabasi Kiomboi ili kujua changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wa madereva wa bodaboda Dkt. Mwigulu amewashauri waendesha bodaboda zao kwa usalama kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali na kukamatwa mara kwa mara na maaskari polisi pindi wanapokosea.
Wafanyabiashara ndogondogo wa Soko Kuu la Kiomboi wamemuomba Mbunge wao kuwasaidia kupunguza kodi nyingi ambazo wanakutana nazo wakati wanafanya biashara katika soko hilo, ombi ambalo Waziri Mwigulu amelipokea na kuahidi kulifanyia kazi.
Vitu alivyosisitiza IGP Sirro akimuapisha Kamishna wa Zanzibar ‘Polisi tuna changamoto’
Aliyoyabaini Naibu Waziri wa Maji katika ziara aliyoifanya DSM